Amani iwe juu yenu na rehma za Allah na Baraka zake..
Karibuni katika chuo cha ibada ya hijja na umrah…
Tunakushukuruni juu ya kuamini kwenu na kusaidia kwenu na kufatilia kwenu, na tunatamani kwenu nyinyi wakati mzuri katika kufahamu elimu ya ibada na hukmu za hijja, umrah na ziara…Flag Arabic

chuo cha mafunzo ya ibada ya hijja (Mnask Academy)

Chuo cha ibada ya hijja na umrah

Chuo cha ibada ya hijja na umrah kwa ajili ya mafundisho ya kielektronic ni sehemu ya kielektronia iliofunguliwa kwa ajili ya kufundisha katika uwanja wa elimu ya kisheria ilio andaliwa na kuongozwa na wizara ya mambo ya kiislamu, daawah na muongozo katika nchi ya Saudi Arabia.

Chombo hiki kina saidia kuleta elimu hiyo katika lugha nane (kiarabu-kingereza-kituruki-kiindonesia-kihausa -kiurdu-ibangali-kiswahili) na zitaongezwa lugha zingine hapo baadae.

Masomo na semina zote zilizotangulia katika chuo (Academia) zimeandaliwa na zimerejewa na wizara na zipo tayari kwa ajili ya wahusika bila malipo.

Kama unahitaji kushiriki katika utaratibu wa mafunzo yetu, mshiriki unatakiwa ajisajili kabla, na mwisho wa kila mafunzo kuna mtihani mfupi kwa ajili ya semina utakapo faulu unaweza kupata shahada ya kukamilisha mafunzo ya kielektronia ya ibada ya hijja na umrah.

Mafunzo ya Matukio

TWAWAAF
5 Masomo
NAKUSHUHUDISHENI YA KWAMBA NIMEWASAMEHE
5 Masomo
NGUZO ZA UISLAM
5 Masomo

simu ya Maombi

Kwa mila za maombi kitaaluma juu ya vifaa smart, unaweza kuhudhuria mafunzo ni rahisi, na Sync na toleo mtandao.

 • Neno la waziri wa mambo ya kiislam, ulinganiaji, na muongozo

  Sifa njema zina mstahiki ALLAH, rehma na amani zimwendee mtume wetu muhammadi na swahaba wake wote. Kwa taufiqi ya ALLAH mtukufu ,wizara ya mambo ya uislamu na ulinganizi,na uongofu katika nchi nay a SAUDI ARABIA imetumia mkusanyiko wa baranamiji za kisasa kwa ajili ya kusherehesha elimu ya ibada ya hijja na umra kwa njia na lugha tofauti tofauti ,na inakuja kazi ya ACADEMIA ya mafunzo ya hijja na umra ilio maalumu katika kueneza elimu na hukumu za hijja na umra na ziyara ,kupitia kazi mpya za kiufundi zinazo lenga kutukuza kauli ya mtume rehma na amani ziwe juu yake"CHUKUENI KUTOKA KWANGU MIMI IBADA ZENU",na itajitahidi ACADEMIA YA MANASIKI katika kuwepesisha elimu ya ibada ya hijja ili ifahamike na iwe fupi,na ili wageni kutoka mbali waweze kuifahamu kupitia ufundi na viunganishi na njia za mawasiliano ya kijamii,ili kuendana sambamba na mendeleo ya haraka,katika ulimwengu wa ufundi wa sayansi,na kufikisha elimu ilikuwepesisha huduma za ufundishaji na kuongoza ili twende pamoja na mitazamo ya viongozi wa nchi na ndoto za SAUDI ARABIA katika kuwahudumia mahujaji na wafanya umra kupitia njia mbali mbali za kisasa. Tunamuomba ALLAH awafanyie wepesi mahujaji waweze kutekeleza faradhi kwa wepesi na ,na aziwafiqishe taasisi na makundi kusimamia juhudi zinazo takiwa kwa wote.kulingana na maelekezo ya MTUMISHI WA HARAMU MBILI TUKUFU, na muheshimiwa NAIBU WAKE MUAMINIFU"ALLAH awatie nguvu"

  Swaleh bin Abdulaziz bin Muhammad al-sheikh
 • Neno la naibu waziri wa mambo ya misikit, ulinganiaji na muongozo

  Tunakukaribisheni katika mradi”wa mafunzo ya hijja na umrah” ambayo tunatoa kupitia mradi huo huduma ya ufundishaji kwa mfumo mpya ili kuwawezesha waislamu katika pande zote za dunia kujua elimu ya ibada ya hijja na umrah na yale yanayo fungamana na safari ya hijja katika elimu yakisheria , wameongoza katika uandaaj wa mafunzo hayo wanazuoni walio bobea katika ulinganiaji wa mafundisho ya kiislamu katika hajj, umrah na ziara, sanjari na vipimo vya kielimu na fani za juu zilizo kita na uzuri wa kazi. Tuna muomba Mwenyezi mungu mtukufu awaafiqishe na awape msaada na kupatia waliosimamia kazi hii kwa juhudi hii. Shukran ziwafikie waheshimiwa wote kwa kushiriki kwao kuzuri katika huduma hii mpya tukiwa tunataraji watu wote kufahamu elimu hii ya academia kwa ufundi wa kisayansi na kuwasiliana na wizara kwa dhamana ya kuendeleza na kukuza huduma.

  Dr.Tawfiq bin abdul aziz assudairiy

Jisajili kwenye orodha yetu ya barua pepe

Faida ya mafunzo ya kielektronia kwa academia

 • mada za kujufunzia zimedhibitiwa na kuhakikiwa

  Vyanzo vya kujifunzia kutokana na alama za kidini vimedhibitiwa na kuhakikiwa na academia na kuegemewa kutoka pande zote muhimu na marejeo rasmi.

 • huduma inatolewa bure

  kujisajili na nyenzo zote za mafunzo, mitihani na shahada na kuhudhuria kielektronia ni bure kwa ukamilifu

 • Kuwezesha nidhamu zote

  Unaweza kuanza na kukamilisha zoezi lako kwa kila chombo kilichowezeshwa kama (Simu ya mkononi,simu za mtelezo,-tablet- nukushi na vibanda vya huduma za jamii )

 • Lugha mbalimbali

  Inakuletea masomo na taratibu za academia na ufundi ya kielektronia kwa lugha nane hadi sasa.

 • Nyakati za mazoezi

  Siku yoyote na wakati wowote asubuhi au jioni unaweza kusajili mahudhurio na kuendelea na mazoezi.

Washirika

Habari mpya kabisa