Background Image

habari zetu

MANASIKI NI ACADEMIA YA KWANZA ILIO ANZISHWA MAKHUSUSI KWA AJILI YA KUFUNDISHA ELIMU YA HIJJA NA UMRA KUTOKA MBALI

MANASIKI NI ACADEMIA YA KWANZA ILIO ANZISHWA MAKHUSUSI KWA AJILI YA KUFUNDISHA ELIMU YA HIJJA NA UMRA KUTOKA MBALI

3:25 am Friday 5th Dhu al-Qi'dah 1438 H

Ameweka wazi muheshimiwa raisi mwenye mamla ya academia sheikh TWALALI BIN AHMADI AL-AQILI kwamba  academia ya manasiki ni moja ya kazi za kitecnologia za wizara ya mambo ya kiislamu,ulinganiaji,na uongofu ya SAUDI ARABIA,akitilia nguvu kua ni kazi ya kitaaluma yenye kufundisha kitecnologia,inajitahidi kueneza elimu ya manasiki na hukumu za   ibada ya hija na umra,na ziara katika nchi tofauti za kiislamu,kupitia mindao ya kisasa.

 

Na inazingatiwa academia ya manasiki kama sehemu ilio fungamana na huduma ambazo zinakujia katika mtiririko unao kwenda sambamba na utaratibu unao letwa na wizara ili kuwafundisha waislamu njia sahihi inayo kubaliana na mafundisho ya mtume katika safari hii ilo barikiwa.

 

Na ametangaza mshauri wa waziri wa mambo ya kiislamu,ulinganiaji,na uongofu sheikh TWALALI  kwamba academia ya manasiki itakua ni gumzo la ulimwengu kwa kuzingatia ndio chuo cha kwanza cha mafunzo- ya ibada ya hijja na umra –kinalenga wale wote wenye kupenda kujua elimu ya ibada ya hijja na umraulimwenguni,na hasa wale wanao penda kufaidika na huduma hii ya bure,amabayo ina leta masomo yake kwa lugha nane za kimataifa,wameshiriki katika kuandaa na kuleta huduma hii kikundi cha walinganiaji wanaofundisha hijja na umra na ziara, wenye kutegemewa kwa ajili ya kazi hii tukufu  ,na miongoni mwao ni kundi katika walio bobea ndani ya kazi hii na wakufunzi.

 

Na akatilia nguvu  AL-AQILI:kwamba academia manasiki ambayo itaanza wiki ya kwanza ya mwezi wa DHUL-QAADA mwaka 1438 hijiria ili wafaidike wageni wa ALLAH wakati wa msimu ujao wa hijja.

 

Akitia mkazo ya kwamba huduma hii inakuja sambamba na umuhimu wa mtumishi wa haramu mbili tukufu mfalme SALMANI BIN ABDUL AZIZI  ALU- SUUDI na naibu wake muaminifu ,na kwa yale yanayo afikiana na ndoto za SAUDI ARABIA za mwaka 2030.

 

Na akaashiria kwamba academia katika marhala yake ya mwanzo itasimamia kufundisha ibada ya hijja na umra kwa lugha za asili kasha itaenea mpaka kufikia kutoa huduma zake kwa lugha zote ulimwenguni.

 

Na akakazia AL-AQILI  kwamba wizara kupitia watu wenye uzoefu katika utumiaji  wa tecnologia na ufundishaji  wamefanya kazi kwa pamoja  katika kuweka misingi ya hii academia kwa ufundi wa hali ya juu na wakawakalifisha kikundi cja watu walio bobea katika uwanja huu na ikapupia kuvumbua na kuanzisha mambo yenye  kuendelea pamoja na kuweka sawa uzoefu,na ukosoaji wenye kuendelea,na uwekaji wa aina tofauti tofautina mawasiliano na mazoezi yanayo kuja kwa ajili ya kuhakikisha ndoto za wizara inayo kusudia kufikisha elimu na kufundisha ibada ya hijja na umra kwa njia za kisasa na lugha mbali mbali,na kuzingatia kua hilo ndio lengo kuu la kazi zote za academia.

Na akakazia kwamaba wizara imejikita zaidi kupitia academia kwa ufahamu wa kazi kwa moyo mmoja na kutafuta  njia nyepesi zaidi  ya kufundisha    ,inayo lenga kueneza taaluma ilio wazi na haraka na yenye kufahamika na nyepesi na fupi na ilio hakikiwa kwa ajili ya kusherehesha nguzo za uislamu zinazoweka weka wazihukumu ya faradhi ya hijja ,na kupamba vizuri utendaji wa kazi ,na kutofautisha njia za mazoezi.

 

Na akaweka wazi kwamba utendaji kazi wa academia unakuja kupitia utaratibu na mtiririko ulio fungamana na mpangilio na njia nzuri,na uliojengwa juu ya   mpango kazi mkubwa unao toa picha ya  juhudi za SAUDI ARABIA katika kutekeleza uwezekano wote wa kuwahudumia wageni wa ALLAH,sambamba na yale yanayo onwa na utawala huu mzuri,

Akibainisha kwamba academia manasiki itafanya kazi kulingana na mpango wa hatua kwa hatua ili kufundisha wale wanao faidika na huduma zake misingi ya wazi katika kufanya ibada ya hiija na umra kama ilivyo kuja katika QURANI NA SUNNAH, pamoja na kulinda utukufu wa  maana ya usawa na uadilifu na utukufu wa nyakati na sehemu,nay ale yanayo fungamana wajibu na nguzo katika hukumu za kisheria.

Na akaweka sheikh TWALALI AL- AQILI malengo ya academia yenye kulenga kueneza tamaduni na  elimu na hukumu za ibada ya hijja na umra kupitia hatua zifuatazo:

 

-kusherehesha ibada ya hijja na umra na ziara kwa kufata njia ya wema walio tanguliana wanachuoni wetu watukufu.

-kutumia njia za kutngaza na habari ili kusherehesha  na kupanua elimu ya ibada ya hijja na umra kwa lugha mbali mbali.

-kusherehesha ufahamu na maana ya nguzo za uislamu,imani,na ihasani,na tabia na historia ya mwenendo wa mtume ,na elimu ya QURANI TUKUFU na kuisherehesha kupitia semina na masomo na vipindi vya television vinavyo onekana na kusikika na kusomwa..

 

Na akafafanua kuhusu malengo yake ni kuiweka  academia manasiki katika chombo  kimoja cha taaluma  kinacho fanya kazi  ambayo itakua na nafasi kubwa katika kueneza uelewa na elimu inayo husiana na ibada ya hijja na umra na nguzo zake na wajibu wake na hukumu zake,na hukumu za itikadi,na sheria  kwa wageni wa ALLAH,na kujitahidi kufanikisha raha zao,na amani yao,na salama yao,na kuwajali na kuwachunga katika kuwaongoza na kuwafundisha..

 

Na akakaziza sheikh AL-AQILI mshauri wa waziri wa mambo ya kiislamu,ulinganiaji,na uongofu ,na waziri wa mambo ya hijja  na umra na habari kwamba academia ital eta huduma zakekupitia “kiwakilishi cha manasiki”bure kaitika pupa yake kukuza mawasiliano ya kiwango kikubwa  cha muhajaji-  wa nyumba ya ALLAH tukufu -kinacho wezekana,na inajitahidi  katika kueneza na kufaidika kupitia huduma ya mawasiliano ya kijamii na kufundisha kupitia na vifaa vya kisasa vyenye uwezo mkubwa ,bila kuzingatia sehemu wanazo patikana watumiaji wa huduma hio  na wakati wa kutumia,kwa lugha ya KIARABU  ,  NA KINGEREZA  ,  NA  KITURUKI  ,  NA  KIINDONEZIA ,NA  KIHAUSA   ,  NA  KISWAHILI  ,  NA KIURDU  ,  NA  KIBANGALI.